Klabu ya Yanga imerejea kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 23 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
- Bao pekee alilofunga kinda Clement Mzize dakika ya 18 ni la kwanza kuifungia Yanga kwenye mechi za Ligi Kuu baada ya kupandishwa timu ya wakubwa msimu huu kutoka timu ya vijana (U-20).
- Ushindi huo unaipeleka Yanga juu kileleni kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 23 sawa na Azam lakini ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku ikiwa na michezo miwili mkononi.
- Yanga imendelea kuboresha rekodi yake ya kucheza michezo mingi ya Ligi Kuu bila kupoteza ambapo leo imefikisha mchezo wa 46 chini ya Kocha Nasredinne Nabi bila kufungwa.
- Kipigo ilichokipata Kagera Sugar ni cha kwanza msimu huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba baada ya kucheza mechi nne za nyumbani kwenye uwanja huo bila kupoteza ikishinda tatu na sare moja huku mchezo pekee wa nyumbani iliokuwa imefungwa ni dhidi ya Singida Big Stars uliochezwa Kaitaba mkoani Kagera.
- Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Kocha Mecky Maxime tangu alipochukua mikoba ya Francis Baraza akiiongoza kwenye mechi mbili akishinda dhidi ya KMC na kupoteza leo mbele ya Yanga.
- Wachezaji Nassoro Ufudu wa Kagera Sugar, na Ibrahim Bacca na Farid Mussa wa Yanga wameonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo katika dakika ya 35 na 90.
- Mchezo huo umechezwa katika mazingira yasiyo rafiki ya uwanja baada ya mvua kunyesha ikisababisha uwanja kuteleza, wachezaji kushindwa kupiga pasi kwa usahihi na kukimbia.
- Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime alifanya mabadiliko kumtoa Datius Peter na kumuingiza Dickson Mhilu, Mbaraka Yusuph na Meshack Mwamita na kuwaingiza Hamis Kiiza na Erick Mwijage.
- Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Joyce Lomalisa na kumuingiza Farid Mussa kisha wakitoka Clement Mzize, Kibwana Shomari na Sureboy na kuingia Bernad Morrison, Djuma Shaban na Khalid Aucho, wakati huo wapinzani wao waliwatoa
- Kagera Sugar imepata penalti dakika ya 70 baada ya kipa wa Yanga, Djigui Diarra kumchezea madhambi Hamis Kiiza huku penalti hiyo ikipigwa na Erick Mwijage lakini Diarra akafanikiwa kuicheza na kuinusuru Yanga.
No Comment! Be the first one.