
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kusogeza mbele droo ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Awali droo hiyo ilikuwa ifanyike kesho Novemba 16 nchini Misri lakini taarifa iliyotolewa na CAF imesema tarehe mpya itatangazwa.
“CAF inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Tanzania inawakilishwa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga Kombe la Shirikisho.
No Comment! Be the first one.