
Dar es Salaam. Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 11 akiwemo kocha wa makipa wa timu ya Simba SC, Muharami Sultan (40) wakiwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi.
Hayo yalisemwa leo Novemba 15 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya amesema kuwa watuhumiwa waliokamatwa na dawa za kulevya aina ya heroine ni kocha wa makipa wa Simba, Muharami Sultan (40), mmiliki wa kituo cha
Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi Seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu Mbonde (54) mkazi wa kisemvule na John John maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy
Wengine ni Rajabu Dhahabu (32)) mkazi wa Tabata, Seleman Matola Said (24) mkazibwa Temeke Wailes, Hussein Pazi (24) mfanyabiashara na Ramadhani Chalamila (27) mkazi wa Kongowe
No Comment! Be the first one.