Mchezaji Bora wa Wiki Caf – Chama Mchezaji Bora wa Wiki Caf
Kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama amechaguliwa kuwa mchezaji bora Wiki ya raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwashinda Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns , Ahmed Zizo kutoka Zamalek na Walid Sabbar wa Raja Casablanca .
Chama ameshinda tuzo hizo baada ya kuiongoza Simba SC katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Vipers SC ya Uganda huku akifunga bao pekee la Wekundu hao wa Msimbazi.
Kuhusu Clatous Chama
Clatous Chama ni mchezaji wa kulipwa wa Zambia ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa Simba S.C. na timu ya taifa ya Zambia. Anajulikana kwa ufungaji wake wa mabao, uchezaji, uongozi, upigaji wa adhabu na kiwango cha kazi
No Comment! Be the first one.