
LONDON, ENGLAND. KIPA wa Chelsea, Edouard Mendy ana wakati mgumu hususan nafasi yake katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Graham Potter kwa mujibu wa ripoti.
Mendy alikuwa na mafanikio mazuri Stamford Bridge tangu aliposajiliwa akitokea Rennes mwaka 2020 kwa kitita cha Pauni 22 milioni lakini sasa mambo yamemuendea kombo.
Nafasi ya Mendy kikosi cha kwanza cha Chelsea imekuwa finyu kwasasa tangu Thomas Tuchel alipofungashiwa virago nafasi yake ikichukuliwa na Graham Potter.
Kipa namba mbili wa The Blues, Kepa Arrizabalaga ndio amekuwa chaguo namba moja la Potter badala ya Mendy baada ya kuumia mguu.
Baada ya kurejea kikosini Mendy alikosa baadhi ya mechi za hivi karibuni Kepa akisimama langoni huku hofu ikitanda huenda hiyo ndio mwisho wa nafasi yake kikosi cha kwanza.
Wakati huohuo taarifa zimeripoti Potter ameanza kumnyemelea kipa Brighton, Robert Sanchez aliyemfundisha wakati alipokuwa huko kabla ya kujiunga na Chelsea.
Mendy anatarajia kuanza kikosi cha kwanza cha Senegal katika fainali za Kombe la Dyunia zitakazoanza wikiendi hii.Hatahivyo Mendy hatauzwa dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Januari mwakani.
Lakini uwamuzi kuhusu hatima utafanyika kwani amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ambao utaisha mwisho wa msimu huu.
Mazungumzo ya awali kati ya Mendy na uongozi wa The Blues haukufikia muafaka mzuri huku Potter akikata tamaa uwezekano wa kipa huyo kubaki siku za usoni kwa mujibu wa ripoti.
No Comment! Be the first one.