
BAADA ya taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa imemkamata Kocha wa Makipa wa Simba Muharami Saidi Sultan kwa tuhuma za madawa ya kulevya, uongozi wa timu hiyo umekanusha kuwa Muharami hakuwa kocha wao.
Shilton ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi kabla ya kuwa kocha wa makipa, anashikiliwa na kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa dawa ya kulevya aina ya Haeroine.
Katika taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Simba inaeleza kuwa Muharami hakuwa muajiriwa, ilimuomba kuwafundisha makipa wa timu hiyo,
“Simba ilimuomba na kukubaliana na ndugu Muharami kuwanoa makipa wetu kwa muda wa mwezi mmoja, wakati klabu ikiendelea kutafuta kocha wa magolikipa” taarifa ilisema.
Simba imeeleza kuwa hawahusiki na tuhuma zinazomkabili Muharami na inawaomba mashabiki kuwa watulivu kwa hakuna athari yoyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyemkumba kocha huyo.
No Comment! Be the first one.